WASAIDIZI WA KISHERIA KWA AJILI YA HAKI ZA MAZINGIRA

Kituo cha Sera na Utafiti- Mpango wa Haki za Mazingira wa Namati
Utangulizi na Maelezo ya Jumla ya Mwongozo wa Utendaji
Maeneo mengi ya dunia, bila kujali viwango vyao vya maendeleo ya kiuchumi,
yapo katika ukingo wa mgogoro mkali wa kimazingira.
Katika maeneo haya, shughuli za miradi ya uzalishaji kama vile mashamba
makubwa, uchimbaji madini na maendeleo ya viwanda zimezorotesha hali za
kiuchumi, kijamii na afya za jamii jirani na zile za mbali pia. Sheria na tasisi zao
imara za kitaifa na kimajimbo zilizopo kwa ajili ya ulinzi na usimamizi wa malighafi
zimebakia kwenye karatasi na ukiukwaji wa sheria umekuwa na athari kubwa
kwenye maisha ya ya jamii, afya, upatikanaji wa ardhi na maisha bora.
Mwongozo wa utendaji wa Namati na CPRS wa wasaidizi wa kisheria wa Haki za
Mazingira ni hatua moja iliyolenga kuziba mwanya huu wa utekelezaji wa
kimazingira.

Mwongozo huu unatoa mbinu kwa wahamasishaji wa jamii, wanaharakati na
makundi ya wananchi waache kutaja tu matatizo na waanze kuchukua
malalamishi yanayoshughulikiwa na taasisi za kimazingira. Mwongozo huu ni
matokeo ya miaka minne ya kazi iliyofanywa na wasaidizi wa kisheria wa Mpango
wa Haki za Mazingira wa CPRS- Namati ili kusaidia jamii athirika kuandikisha
malalamishi na kutafuta suluhu katika kesi zaidi ya 150 za ukiukwaji huko India.
Tunatarajia kwamba mwongozo huu utayasaidia mashirika ya mitaa na makundi
ya kijamii kuishughulikia migogoro ya kimazingira na kuwatafutia utatuzi wale
walioathirika.

This resource is also available in FrenchOriyaHindiGujaratiKannada, and Bahasa Indonesian.

Share:      
Uploaded on: Oct 05, 2018
Issues: Community Paralegals, Environmental Justice, Governance, Accountability & Transparency, Policy Advocacy Tool Type: Manuals & Guides Method: Improving Governance, Accountability and Transparency, Navigating Administrative Processes, Negotiating with Private Firms Languages: Swahili Regions: > Global